Jumanne, 7 Julai 2015

VIAMBISHI TAMATI MAANA VYA KISWAHILI

Viambishi tamati– Hivi hudokeza kauli mbalimbali za vitenzi. Mfano: - Anacheza – kutenda Unachezwa- Kutendwa Utachezewa- Kutendewa Nimemlia- Kutendea Wamewasomesha- Kutendesha n.k
Mzizi Kiambishi Kiambishi tamati maana Neno jipya Kauli Viambishi vya kauli Chez a Cheza Kutenda -a e a Chezea kutendea -e- / -i- Pig ian a Pigiana Kutendeana -ian-/-ean- iw a Pigiwa Kutendewa -iw-/ew- Som esh a Somesha Kutendesha -ish-/esh- eshw a Someshwa Kutendeshwa -ishw-/eshw- Lim ik a Limika Kutendeka -ik-/-ek- an a Limana Kutendana -an- w a Limwa Kutendwa -w-
Viambishi tamati katika vitenzi vya Kiswahili.
Viambishi tamati katika lugha ya Kiswahili hujitokeza kudokeza dhima kubwa mbili:- I. Viambishi tamati vya kauli II. Viambishi tamati maana
Kiambishi tamati maana – Hii ni mofimu ya mwisho kabisa katika kitenzi yenye dhima ya kukamilisha maana kusudiwa na msemaji wa tungo hiyo. Mfano:- Pig-a, Chez-w-a, Som-esh-a n.k. Mofimu hizi hujitokieza mbele ya viambishi vya kauli au mbele ya mzizi wa neno lenyewe.
Aina za viambishi tamati maana. Viambishi tamati maana vinajitokeza katika aina tofauti mbili ambazo ni; Viasili na Vijenzi.
1. Viambishi tamati maana viasili Hivi ni vile vinavyojitokeza katika shina asilia la kitenzi husika. Viambishi hivi vipo katika makundi mawili:- a) Vyenye asili katika lugha Kiswahili, hivi huwa ni mofimu (-a) Mfano; Pig-a, Chez-a, Omb-a n.k b) Vyenye asili katika lugha za Kigeni, hivi huwa ni mofimu (-i), na (-u) Mfano; Sal-i, Shukur-u n.k.
2. Viambishi tamati maana vijenzi Hivi ni vile ambavyo hujitokeza katika vitenzi vilivyonyambulishwa. Viambishi hivi hujitokeza kukamilisha dhima zifuatazo:- a) Viambishi tamati maana vikanushi, hivi hukamilisha maana iliyokusudia kuonesha ukanushi wa tendo, huwa ni mofimu (-i) Mfano; Sichez-i, Huimb-i, Hawasom-i, Silal-i N.k b) Viambishi tamati maana Vielekezi, hivi hukamilisha maana iliyokusudia kuelekeza jambo, kitenzi hicho huwa na mofimu ya masharti Ka- na mofimu elekezi huwa ni mofimu (-e) Mfano; Kachez-e, Kasom-e, Kalim-e, Kaog-e N.k c) Viambishi tamati maana Vinominishi, hivi ni vile vinavyobadili kitenzi kuwa nomino, huwa ni mofimu (-aji), (-zi), (-shi), (-o) Mfano; Mchez-aji, Mwi-zi, Mche-shi, Pig-o N.k

Maoni 1 :

  1. Ahsante sana kwa darasa hili,umejitahidi kueleza vizuri na nina amini itawasaidia wengi

    JibuFuta