1.
Nini
maana ya fasihi? Bainisha tanzu na dhima za Fasihi.
- Swali hili linamhitaji mwanafunzi aeleze maana ya fashi kisha ataje na kueleza aina mbili za fasihi yaani Andishi na Simulizi na amalize kwa kueleza umuhimu wa fasihi kwa ujumla wake. Hivyo linaweza kujibika kama ifuatavyo:-
Fasihi
ni sanaa ya kutumia lugha ili kuwakilisha wazo Fulani kwa hadhira kusudiwa.
Sanaa ni ufundi wa kipekee unaokusudia kufanya kitu Fulani kivutie na kupendeza
machoni mwa watu. Hivyo tunaposema kuwa fasihi ni sanaa ya lugha ina maana kuwa
fasihi huipamba lugha ya kawaida kuonekana isiyo ya kawaida ili kuwavutia watu
na kuwakosha kihisia. Si kila mtu anaweza kuwa msanii wa fasihi hivyo huwa kama
tunu kwa mtu yaani kipaji.
Fasihi
imegawanyika katika tanzu kuu mbili:-
i.
Fasihi Simulizi. Utanzu huu wa
fasihi ulianza tangu kuwepo kwa mwanadamu. Mwanadamu asingeweza kuishi vyema
katika mazingira yake kijamii bila kuwasiliana, na ili kuwasiliana alihitaji
lugha. Lugha ilitumika pia katika maburudisho mbalimbali na huo ndio ukawa
mwanzo wa fasihi pia. Hivyo utanzu huu wa fasi ulianza tangu kuwepo kwa
mwanadamu. Utanzu huu hutumia lugha ya masimulizi katika kufikisha ujumbe wake
kwa hadhira kusudiwa. Kwa kusema hivyo kumbe; Fasihi simulizi ni utanzu wa fasihi utumiao lugha ya masimulizi ya
mdomo kujikamilisha kidhima.
ii.
Fasihi Andishi. Utanzu huu
ulianza baada ya mwanadamu kuvumbua alama zinazowakilisha sauti za lugha yake.
Alama hizo hujulikana kama andishi. Maandishi ni alama zinazowakilisha maumbo
ya sauti ya mwanadamu. Kila lugha ina alama zinazowakilisha sauti za lugha
hiyo. Hivyo utanzu huu ulikuja baada ya utanzu wa fasihi simulizi kuwepo. Fasihi andishi ni utanzu utumiaolugha ya
maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira kusudiwa.
- Fasihi
huwa na kazi mbalimbali katika jamii. Na zifuatazo ni miongoni mwa kazi nyingi
za fasihi katika jamii, lakini lazima izingatiwe kuwa fasihi hulenga kufikisha
wazo Fulani la msanii kwa hadhira kusudiwa hivyo wazo hilo linaweza kuwa la:-
Kuonya na kuadilisha jamii.
Fasihi ina kazi ya kufichua mabaya na mazuri yanayotendeka katika jamii husika
na haihishii hapo lakini pia hutoa maonyo juu ya mabaya hayo na zaidi kusifia
na kuendeleza mazuri yote yaliyopo katika jamii husika, lengo ni kuimarisha
utamaduni na maadili katika jamii. Iwapo watajitokeza watu Fulani wanaoenda
kinyume na matakwa ya jamii, fasihi ina wajibu wa kuwasema waziwazi na kuwaonya
juu ya mienendo yao huku ikiwarekebisha kifikra pia.
Kuelimisha jamii.
Fasihi inalo jukumu la kutoa mafunzo mbalimbali kwa jamii. Mafunzo
yanayorekebisha tabia na kudumisha utamaduni. Siku zote fasihi hulenga kuchunguza
mambo yote yanayoendelea katika jamii mazuri na mabaya, kwa kuzingatia matukio
ya kihistoria, hivyo huwa ni kazi ya waandishi na wasanii kuiandikia jamii ili
kuelewa kile kinachoendelea ndani ya jamii kwa mapana na marefu ili asiwepo
hata mwanajamii mmoja atakayekuwa nyuma ya wakati kwa kila matukio yanayojiri
ndani ya jamii husika.
Kuwaburudisha wanajamii.
Burudani ni hali ya kuamsha hisi za furaha za mwanadamu. Wasanii wengi hulenga
suala hili. Ndivyo fasihi ilivyo, mtu huamishwa kihisia pale alipo na kufanywa
kuwa kati8ka anga la furaha baada ya kusoma kazi ya fasihi. Msanii
asiyefanikiwa katika suala hili basi inaaminika kuwa anayo mapungufu makubwa
katika kazi yake na inajumuishwa kuwa hajafaulu kuiteka hadhira yake.
Kulinda na kuhifadhi amali za jamii
husika. Utamaduni ni hali halisi ya maisha ya jamii
Fulani, jumla ya imani katika mavazi yao, dini yao, lugha yao, miiko yao,
maadili yao na desturi zao. Hivyo fasihi
huwa na kazi ya kulinda jumla hizo na kuziendeleza ili ziwepo vizazi hata
vizazi.
Kudumisha na kuendeleza lugha.
Fasihi hutegemea lugha kama zana ya kufikisha ujumbe kwa hadhira kusudiwa.
Hivyo ni njia nzuri tu ya kukuza na kuimarisha lugha ya jamii husika kwa kuwa
njia kuu ya uwasilishwaji wake ni lugha. Maneno mengi yanayotumiwa na wanajamii
yana mwanzo wake kutoka kwa wasanii wa mashairi, riwaya, tamthiliya, nyimbo na
hata sanaa za maonesho.
Hivyo
ni wazi kuwa fasihi ina wajibu mkubwa sana katika jamii kama inavyodhihirishwa
katika hoja hizo hapo juu. Lakini izingatiwe kuwa ili fasihi kuwa fasihi lazima
iwe na sifa zifuatazo, iwe na ufundi, ufundi huo uwe wa lugha, lugha
inayoelezea kinachotendeka katika jamii
na maelezo hayo yawe na fani na maudhui. Hizo ndizo sifa za Fasihi.
2.
Fasihi
simulizi na Fasihi andishi hutofautiana kitanzu. Fafanua kauli hii.
- Swali hili linakusuduia mwanafunzi aweze kueleza bayana tanzu za fasihi simulizi na fashi andishi zinavyotofautiana.
Fasihi
simulizi ni utanzu wa fasihi unaowasilisha ujumbe wake kwa njia ya masimulizi ya
mdomo, ilhali fasihi andishi ni ule utanzu wa fasihi unaowasilishwa kwa njia ya
maandishi katika machapisho. Si
uwasilishwaji tu unaoleta utofauti wa fasihi andishi na simulizi lakini pia
tanzu zao hutofautiana. Zifuatazo kwanza ni tanzu za fasihi simulizi:-
Hadithi.
Ni tungo za kifasihi zitumiazo lugha ya nathari. Lugha ya nathari ni lugha ya
mjazo inayotumiwa katika matumizi ya kwaida ya kilan siku. Masimulizi hayo huwa
yanakuwa katika mtiririko maalum unaokamilisha visa. Vipera vya Hadithi ni
kama; Ngano – ambazo huwa ni hadithi
za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, mimea na watu kufikisha ujumbe, Vigano – huwa hadithi fupi zinazxolenga
kuadilisha zaidi, Soga – ni hadithi
fupi zinazolenga kukejeli na kuchekesha, Tarihi
– husimulia matukio ya kihistoria yanayobuniwz au yale yaliyotokea kweli, na Visasili – ni hadithi zinazotumia
wahusika mbalimbali kama watu na miungu.
Semi.
Ni fungu la tungo la fasihi simulizi ambazo huwa ni fupifupi zinazotumia picha,
tamathali za semi na ishara. Huwa na aina zifuatazo; Methali – hueleza kwa ufupi fikra au mafumbo yaliyomo kwenye fikra
za mwanadamu, Vitendawili – ni usemi
uliofumbwa ambao hutolewa ili ufumbuliwe, Nahau
– ni misemo ya picha ambayo huleta maana iliyofichika, Misemo – ni fungu la maneno linalotumiwa na jamii ya watu kwa namna
maalumu ili kutoa maana Fulani, Mizungu
– ni kauli yenye picha za mafumbo na inayoonesha ukinzani wa fikra au
tukio.
Ushairi. Ni
fungu linalojumuisha tungo zote zenye mapigo ya kimuziki yaliyopangwa kwa
utaratibu maalumu mathalani yakiwa yamepangwa kwa muwala wa urari. Ushairi huwa
na aina hizi; Nyimbo – Ni kile kinachoimbwa yaani hali ya kupanda na kushuka
kwa sauti kimuziki, Maghani – ni ushairi unaotolewa kwa kalmia badala ya
kuimbwa, Ngonjera – huwa na muundo wa mashairi ya kimapokeo na hutumia lugha ya
mazungumzo ya majibishano baina ya watu wawili au zaidi.
Sanaa za maonesho.
Ni sanaa ambazo uzuri wake unajkitokeza katika umbo lakudumu ambalo huweza
kuoneshwa muda wowote kama vile
uchongaji, uchoraji, udarizi, ufinyanzi n.k. Sanaa za maonesho hujitokeza
kupitia; Matambiko – hii ni sanaa ya maoneshop ambayo huusisha utoaji wa sadaka
zinazoelekezwa kwa Mungu, miungu, mizimu hata mapepo, Majigambo – ni snaa ya
maonesho ambayo mtu hutoa masimulizi ya kujigamba kuhusu ushujaa wake nay ale
aliyoyatenda maishani mwake, Miviga – ni sherehe zinazofanywa na jamii Fulani
kwa lengo la kufundisha vijana na hufanyika katika kipindi maalumun kila mwaka,
Ngoma – huusisha uchezeshaji nwa viungo vya mwili wenye kuzingatia upekee wa
mdundo na miondoko maalumu.
Fasihi
Andishi imepata tanzu zake kutokana na fasihi simulizi, kwa maana kwamba kila utanzu
uliopo katika fasihi andishi una chimbuko lake katika fasihi simulizi sema tu
umebadilishwa kwa kuwekwa katika mpangilio maalumu wa kimamaandisahi. Zifuatazo
ni tanzu za fasihi Andishi:-
Riwaya.
Riwaya imetokana na hadithi katika fasihi simulizi, hivyo ni hadithi ndefu
zenye ubunaji ndani yake ambazo kwa mawanda mapana huwasilisha ujumbe wake kwa
hadhira kwa kutumia lugha nathari ambayo huwa na mchangamano wa visa na matukio
yanayomulika maisha halisi ya jamii husika.
Tamthiliya.
Imetokana na sanaa za maonesho katika fasihi simulizi, ni utungo wa kimchezo wa
kuigiza yaani drama ambao unawasilishwa kupitia maandishi. Tamthiliya huweza
kuigizwa jukwaani kwani huandikwa kwa kudhihirisha matendo na majibizanon ya
wahusika hivyo ina mtindo wa lugha ya majibizano yaani dailojia.
Ushairi.
Huu umetokana na utanzu wa ushairi katika fasihi simulizi, ambapo ni sanaa
inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye mvuto, hutumia
lugha ya mkato, na kunakuwa na matumizi ya lugha ya picha na ishara ili kueleza
wazo, vilevile huweza kuimbika. Hivyo kutokana na hayo ushairi ni sanaa
inayoambatana na kuibua hisia kutokana na ulimwengu ambyo hutumia lugha ya
mkato na yenye urari kimuundo.
Kwa
hiyo basi ni msingi tu kutambua kwamba tanzu mbili za fasihi yaani fasihi
simulizi na fasihi andishi zinatofautiana kitanzu, kwa kuwa fasihi simulizi ina
tanzu nne wakati fasihi andishi ina tanzu tatu, na pia fasihi andishi imezipata
tanzu zake kutoka katika fasihi simulizi.
3.
Fafanua
vigezo tofauti tofauti vinavyoleta utofauti katika tanzu mbili za fasihi.
v Swali
hili linamhitaji mwanafunzi wa kueleza tofauti ya fasihi andishi nan fasihi
simulizi.
Fasihi
ni sanaa itumiayo lugha katika kufikisha ujumbe kwa hadhira kusudiwa, ikiwa na
tanzu mbili, tanzu hizo hutofautiana katika vipengele vifuatavyo kama
inavyoonekana katika jedwali hili hapa chini:-
KIPENGELE
|
FASIHI SIMULIZI
|
FASIHI ANDISHI
|
|
1. Umri
|
Ni kongwe kwa kua imeanza mara baada
tu ya chimbuko la mwanadamu.
|
Ni matokeo ya fasihi simulizi, hivyo
ni changa bado maana ni zao la fasihi simulizi.
|
|
2. Uhifadhi
|
Uhifadhiwa kichwani kabla ya kuanza
pia kuhifadhiwa katika vinasa sauti baada ya mabadiliko ya sayansi na
tekinolojia.
|
Huifadhiwa katika maandishi.
|
|
3. Uwasilishwaji
|
Huwasilishwa kwa masimulizi ya mdomo.
|
Huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
|
|
4. Umiliki
|
Ni mali ya jamii.
|
Ni mali ya msanii.
|
|
5. Hadhira
|
Ni watu wote katika jamii
|
Ni wale wajuao kusoma pekee.
|
|
6. Tanzu
|
Huwa na tanzu nne yaani; semi,
hadithi, ushairi na sanaa za maonesho.
|
Huwa na tanzu tatu yaani; ushairi,
tamthiliya na riwaya.
|
|
7. Mabadiliko
|
Hubadilikia kwa haraka kulingana na
mahitaji ya hadhira.
|
Hudumu katika hali ileile kwa muda
murefu.
|
|
8. Utendaji
|
Huambatana na utendaji.
|
Hakuna utendaji.
|
|
4.
Uhifadhi
wa kazi ya fasihi simulizi umegawanyika katika njia tofauti tofauti, zielezee.
- Swali hili linamhitaji mwanafunzi azielezee njia mbalimbali za kuhifadhi fasihi simulizi. Sweali hili linawezxa kujibika kwa mfumo ufuatao:-
Fasihi
simulizi ni sanaa ya lugha inayowasilishwa kwa njia ya masimulizi yam domo.
Fasihi simulizi ni moja kati ya tanzu mbili za fasihi na huu ndio utanzu
mkongwe zaidi kuliko ule wa fasihi andishi. Fasihi simulizi huweza kukusanywa
na kuhifadhiwa kupitia njia zifuatazo:-
Kichwa.
Tangu awali, fasihi simulizi imekuwa ikihifadhiwa kichwani mwa fanani na
kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Hii imekuwepo tangu
mwanzo fasihi ilipoanza na ndio sababu imekuwa ikirithishwa kizazi hata kizazi
kupitia masimulizi hayo ya fanani kwenda kwa hadhira ambayo hutoka moja kwa
moja katika chopmbo cha kuhifadhia yaani kichwa.
Kanda za kunasia sauti.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia fasihi simulizi imeweza kuhifadhiwa
katika kanda za kunasia sauti, hii njia inasaidia fasihi kufikishwa kwa muda na
mahali popote bila ya kuwepo na fanani hai.
Maandishi.
Fasihi simulizi
asante
JibuFutafasihi simulizi huweza kupotea haraka kwa vile mara nyingi huhifadhiwa kwa kutumia kichwa.
JibuFutaJe tofauti kati ua lugha ya kifasihi na lugha isiyo ya kifasihi ni ipi
JibuFutaTofauti kati ya lugha ya kifasihi na lugha isiyo yakifasihi
JibuFutaVany
FutaTofauti kati ya lugha ya kifasihi na lugha isiyo yakifasihi
JibuFutaNaomba kujua chimbuko la fasihi
JibuFutaMaria
FutaTanzu za fasihi andishi ni zao la fasihi simulizi.Thibitisha dai hili kwa mifano bayana
JibuFutakazi ya wizi weka marejeleo
JibuFuta"Umuhimu wa kazi za fasihi, hutofautiana kutegemeana na utanzu husika" jadili hoja hii kwa kutumia tamthiliya na Riwaya.
JibuFuta