Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru.
Silabi huru ni
zile ambazo huishia na irabu.
Kwa
mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
Silabi funge ni zile zinazoishia na
konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii
inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa
kutoka katika lugha nyingine.
Kwa mfano; Alhamisi – a-l-ha-mi-si
Taksi - ta-k-si
Miundo
ya Silabi za Kiswahili
a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo
maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi.
Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k.
b. Muundo wakonsonanti pekee (K) – Kiswahili
hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa maneno machache
ambayo huwa ni ya nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama mwanzoni au katikati
ya neno. Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi = Nchi n.k
c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) –
Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k.
d.
Muundo
wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo
huukonsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni
kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
e.
Muundo
wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii
hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa,
Tindwa,
Mbwa,
n.k.
f.
Muundo
wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache
ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il-ha-li = Ilhali, Lab-da
= Labda
kazi nzuri
JibuFutanjema
FutaAlhamisi ina silabi ngapi
JibuFutaNNE
FutaKuliundiwa ina silabi ngapi?
JibuFutakevin
FutaKiswahili kipana kweli.
JibuFutatatu
JibuFutaSilabi katika mwafrika
JibuFutaTatu
FutaNaomba mnisaidie umuhimu wa silabi
JibuFutaTaja
JibuFutamaumbo ya silabi za KISWAHILI
Desta Deus
FutaStaftahi ina Silabi ngap
JibuFutaMeshack
FutaTatu
FutaNeno 'Nchi' lina silabi ngapi?
JibuFutamoja
FutaMoja
FutaKutokana na mkazo unaotiwa kwa sauti 'N' hivyo kutamkwa kama nn, neno hili linatupa silabi mbili; n+chi
FutaAsanteni sana
JibuFutaUnda nomino mbili zitokanazo na kitenzi samehe
JibuFutaMOSES OMBENGI RICHARD
FutaMOSES OMBENGI RICHARD
FutaUnda nomino mbili zitokanazo na kitenzi samehe
JibuFutaMsamaha
FutaKusamehe_ nomino kitenzi_jina
neno mbwa lina silabi ngapi
JibuFutamoja
FutaM+ bwa_2
FutaUfafanuzi upo vizuri shukrani sana
JibuFutaKiswahili ni bahari pana
JibuFutaKazi nzuri
JibuFutaNeno blanketi Lina silabi ngapi?
JibuFutaVipi kuusu maumbo ya sarufi za kiswahili sanifu?
JibuFuta